Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchi za Afrika zamulika takwimu kuboresha kilimo na lishe

Nchi za Afrika zamulika takwimu kuboresha kilimo na lishe

Wataalamu wa kilimo na lishe wanakutana huko Rabat, Morocco wakiangazia jinsi ya kuimarisha upatikanaji wa takwimu bora na zenye umuhimu kuhusu lishe na kilimo. Suala hilo limeonekana ni muhimu kwa Afrika wakati huu ambapo bara hilo linahaha kutunga sera bora za kushughulikia tatizo sugu la ukosefu wa chakula. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Mambo hayo ndiyo yaliyojitokeza zaidi katika wakati timu ya wataalamu kutoka nchi 35 wakikutana kwa kikao cha 23 cha kamishana ya afrika juu ya takwimu za chakula

Shirika la chakula na kilimo FAO linasema kuwa  mambo hayo yanapaswa kuzingatiwa kwani kuwepo kwa takwimu sahihi na zinazopatikana kwa wakati kunasaidia  kutoa picha halisi juu ya usalama wa chakula na kilimo ulivyo

Shirika hilo limeongeza kuwa takwimu hizo pia zitatoa mwanga halisi kuhusiana na hali ya usalama wa chakula na kilimo kama hali hiyo inatoa athari ya moja kwa moja katika maeneo kama  mazingira, shughuli z akiuchumi na maisha ya kijamiii kwa ujumla. Sangita Dubey ni afisa wa FAO katika kitengo cha takwimu

(Sauti ya Sangita)

Ama FAO inasisitiza  haja ya kumulika matumizi ya serikali kama yanakwenda sambamba na maazimio yaMaputoya mwaka 2003 ambayo ilizitaka nchi wanachama kutenga asilimia 10 ya matumizi yake kwa ajili ya chakula na kilimo.

Kwa mujibu wa takwimu za sasa ni nchi chache tu ambazo zinakwenda sambamba na azimio la Maputo.Nchi hizo ni pamoja naBurkina Faso,Ethiopia,Ghana,Guinea,Malawi,Mali,Niger na Senegal.