Mawaziri wa WTO wasifu kasi ya kuridhia makubaliano kuhusu mpango wa manunuzi serikalini

4 Disemba 2013

Huko Bali, Indonesia kando mwa mkutano wa tisa wa shirika la biashara duniani, WTO, mawaziri wa nchi wanachama wa makubaliano ya pamoja kuhusu manunuzi serikalini wamesifu kasi ya uridhiaji wa marekebisho ya makubaliano hayo na hivyo kutia matumaini kuwa yataana kutumika mapema iwezekanavyo. Flora Nducha na ripoti kamili

 (Taarifa ya Flora)

Mkurugenzi Mkuu wa WTO Roberto Azevêdo akihutubia kikao cha mawaziri hao amesema makubaliano hayo yaliyopitishwa mwezi Machi mwaka jana na yanapanua wigo wa ushiriki, uwajibikaji na utawala bora katika manunuzi ambapo unawezesha kuokoa kati ya dola bilioni 80 hadi 100 kila mwaka.

Lengo ni kuingiza ushindani wa kimataifa kweye mipango ya manunuzi serikalini na kuhakikisha mchakato ni wa uwazi na unazingatia sheria na kuepusha ubaguzi kwa misingi ya bidhaa, huduma au msambazaji.

WTO inasema kuwa makubaliano hayo yataanza kutumika pindi theluthi mbili za nchi 15 wanachama zitakaporidhia ambapo hadi sasa ni saba tu zimefanya hivyo. Pande hizo ni Liechtenstein, Norway, Canada, Taipei. Marekani, Hong Kong na Umoja wa Ulaya.