Usimamizi bora wa maliasili waweza kukomboa Afrika kutoka umaskini:IMF

4 Disemba 2013

Usimamizi bora wa maliasili barani Afrika unaweza kuwa ni suluhisho la kudumu la umaskini barani humo, na hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la fedha duniani, IMF kama anavyoripoti Jason Nyakundi.

RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Mali asili ndiyo kiungo mihimu hususan kwenye nchi zenye kipato cha chini ambapo huchukua asilimia 36 ya utajiri wa nchi kwa mujibu makadirio ya shirika la fedha duniani IMF.

Mkutano ulioandaliwa mjini Nairobi Kenya umewaleta pamoja mawaziri kutoka Afrika, wanauchumi maarufu, wanasayansi na wataalamu wa masuala ya maendeleo ambao wanajadili njia ya kutumia mali asili kwney maendeleo.

Mkurugenzi mkuu wa shirika la mazingira la Umoja UNEP Achim Steiner amesema kuwa usimamizi bora wa mali asili ni nguzo muhimu ambapo maendeleo  yanaweza kupatikana.

Steiner amesema kuwa bara la Afrika lina mali asili ambayo ni haba kwenye sehemu nyingi za ulimwengu akiongeza kuwa ikiwa mali hiyo itasimamiwa kwa njia nzuri  itainua uchumi wa bara la Afrika .