Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti mpya yatoa suluhu kupunguza mwanya wa chakula duniani

Ripoti mpya yatoa suluhu kupunguza mwanya wa chakula duniani

Hatua madhubuti zinahitajika ili kuboresha uzalishaji wa chakula ili kundoa mwanya wa asilimia 70 uliopo duniani. Utafiti mpya uliofanywa umeangazia baadhi ya suluhu  katika kukabiliana na mahitaji ya chakula yanayozidi kuongezeka duniani.

Tathmini hiyo inaeleza kuwa ulimwengu utahitaji asilimia 70 zaidi ya chakula kuweza kulisha watu bilioni 9.6 ifikapo mwaka 2050. Kwenye miongo kadha inayokuja ulimwengu huenda ukakabiliwa na changamoto nyingi ukihitajika kuziba mwanya uliopo wa asilimia 70 kati ya chakula kitakachohitajika na kile kilichopo. Ripoti hiyo inaeleza kuwa kuongeza uzalishaji wa mimea na mifugo  kwenye ardhi iliyopo sasa kutachangia pakubwa katika  kuzuia uharibifu wa misitu na kupunguza gesi zinazochafua mazingira. Ripoti hiyo inaonyesha kuwa  uzalishaji wa mazao ya kilimo utahitaji kuongezeka kwa asilimia 32 kwa kipindi cha miongo minne inayokuja ili kuzuia ukataji zaidi wa miti.