Usambazaji misaada Syria watia moyo, hatua zaidi zahitajika: OCHA

3 Disemba 2013

Mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na usaidizi wa binadamu, OCHA, Bi. Valerie Amos amelieleza baraza la usalama la Umoja wa Mataifa juu ya kuwepo kwa matumaini  ya kupanuka kwa wigo wa usambazaji wa misaada ya kibinadamu nchiniSyriakufuatia taarifa ya Rais wa barazahiloya tarehe Pili Oktoba mwaka huu.

Taarifa hiyo kuhusu hali ya kibinadamu nchiniSyriailitaka pande zote husika kusitisha chuki na kutoa fursa kwa operesheni za kibinadamu, na hivyo hivyo baada ya kutoa taarifa yake kwa wajumbe wa baraza la usalama, Bi. Amos aliwaeleza waandishi wa habari kuwa…

Tumeshuhudia maendeleo ya kutia moyo katika taratibu za kiutawala zilizowekwa. Mathalani serikali ya Syria imesema zaidi ya vibali 50 vya kuingia vitatoelewa kwa kuzingatia sifa ya mtu husika, na vimeanza kutolewa ninapozungumza. Pia wameturuhusu kufungua vituo vitatu vya ziada ndani ya Syria, lakini ni viwili tu vitakuwa kwa msaada kwetu, kwani cha tatu kilichopendekezwa Al sweda hakitatuwezesha kufika upande wa magharibi wa Daraa mbako ndiko kuna jamii tusizoweza kufikia.”

Amesema serikali na upande wa upinzani wametaja nani watakuwa washauri wakuzunguzma na OCHAkamanjia ya kurahisisha ufikishaji wa misaada. Bi Amos akaulizwa hali halisi ya wahitaji iko vipi hususan wale ambao hawawezi kufikiwa na misaada.

Takribani watu Laki Mbili na Nusu wako kweney maeneo yanayoshikiliwa, hizi ni j amii ambazo hatuwezi kufikai kabisa. Na watu Milioni mbili na nusu wako maeneo ambayo ni magumu kufika, kwa hiyo pengine wamewahi kupatiwa msaada mara moja tu bila nyongeza tena.”

Mkuu huyo wa OCHA amelikumbusha baraza la usalama juu ya umuhimu wa kuhakikisha usalama wa raia na kwingineko ili usaidizi wa binadamu uweze kutekelezwa.