Mabadiliko ya sheria ya jumuiya za kijamii Kenya yatakuwa na athari:UM

3 Disemba 2013

Kundi la wawakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu  leo wameitaka serikali ya Kenya kuipinga sheria itakayoweka vikwazo vigumu kwa jumuiya za kijamii.

Mswada huo ni ushahidi dhahiri kwa kuongezeka kwa mwenendo wa mataifa ya Afrika na kwingineko ambako serikali zinajaribu kuchukua udhibiti zaidi wa makundi huru kwa kutumia kile wanachi walikiita sheria za NGO’s wameonya wawakilishi hao.

Mswada huo wa sheria ambao uliwasilishwa bungeni Kenya tarehe 30 Oktoba ukipitishwa utafanyia marekebisho ya sheria ya  mwaka 2012 mashirika umma yenye manuu na hivyo kuipa uwezo serikali wa kukataa kuyasajili mashirika hayo yakiwemo yale yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s, kuchukua asilimia 15 ya bajeti nzima na kuhakikuisha mashirika hayo yanapitishia fedha za ufadhili wao kupitia serikali kuliko kwenda moja kwa moja kwa mashirika husika.

Kwa mujibu wa Margaret Sekaggya mmoja wa wawakilishi hao mabadiliko ya sheria hiyo yatakuwa na madhara makubwa kwa jumuiya za kijamii Kenya ikiwa ni pamoja ya zile zinazohusika na masuala ya haki za binadamu

Wawakilishi hao wameitaka serikali ya Kenya kusitisha mara moja mchakato wa mswada huo na kutathimini upya kwa kuzingatia sheria za kimataifa za haki za binadamu na viwango vya kimataifa.

Naye Frank La Rurue mwakilishi wa kuchagiza na kulinda haki za maoni na uhuru wa kujieleza amesema sheria hiyo ikifanyiwa mabadiliko itawanyima watu haki ya uhuru wa kukusanyika, wa moani na kujieleza.