Ondoa vizuizi, fungua milango, jumuisha walemavu katika maendeleo: Ban

3 Disemba 2013

Leo ni Siku ya Kimataifa ya watu wenye ulemavu, na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa wito viondolewe vikwazo ili kuhakikisha kuwa takriban watu bilioni moja wanaoishi na ulemavu kote duniani wanajumuishwa katika jamii kikamilifu. Joshua Mmali ana taarifa kamili

Ujumbe wa Katibu Mkuu ulopambwa kwa video maalum, umeenda sambamba na kauli mbiu ya siku hii: vunja vikwazo, fungua milango kwa jamii jumuishi na maendeleo kwa wote:

“Tufanye kazi pamoja ili kila mtu popote pale awe na fursa ya kutimiza ndoto zao na kutumia vipaji ambavyo wamepewa. Tupigie debe maendeleo yanayowajumuisha walemavu, tutoe msisimko kwa mabadiliko mashinani na kuhakikisha maisha ya utu kwa wote”

Na hapa kwenye Umoja wa Mataifa, kumefanyika hafla maalum ya kuadhimisha siku hii kwa hotuba na vitumbuizo.

CLIP

Rais wa Baraza Kuu, John William Ashe, amesema wengi wa watu wenye ulemavu kote duniani wanaishi katika nchi zinazoendelea, katika ufukara, hukabiliwa na ubaguzi na kunyimwa fursa za kimsingi za ukuaji. Ametoa wito wa kuunga mkono kuweka usawa wa fursa kwa watu wenye ulemavu.