Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yalazimika kupunguza huduma zake nchini DRC kutokana na ukosefu wa fedha

WFP yalazimika kupunguza huduma zake nchini DRC kutokana na ukosefu wa fedha

 Shirika la mpango wa chakula duniani WFP  limesema kuwa litalazimika kupunguza baadhi ya huduma zake kuanzia mwezi huu kwenye Jamhuri ya Kidemokrasi yaCongohatua ambayo itawaacha maelfu ya watu bila msaada wowote. Flora Nducha na taarifa kamili.

(RIPOTI YA FLORA NDUCHA)

Ilikuendelea na oparesheni zake kwa kipindi cha miezi sita inayokuja WFP inahitajia dola milioni 75 kwa dharura zitakazoiwezesha kutoa huduma zake hadi mwezi Mei mwaka 2014. Kwa kipindi cha miezi sita uhaba wa fedha unamaanisha kuwa WFP imepunguza migao ya chakula kwa watu waliohama kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini wakati  kunaposhuhudiwa upungufu mkubwa wa chakula maeneo ya mashariki mwa DRC. Kulingana na makadirio yaliyofanywa na  utawala wa mkoa wa Kivu Kaskazini na WFP yanaonyesha kuwa familia sita kati ya familia kumi hazina usalama wa chakula. Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP

(Sauti  ya Byrs)

Kwenye majimbo ya Kivu Kaskazini na Kusini pamoja na Orientale watu Laki tano wasio na uhakika wa chakula kwa bahati mbaya  wataathirika zaidi na uhaba huu wa fedha unaotukabili.  Kwa hiyo itaathiri mgao wa siku wa chakula kwa maelfu ya watoto wa shule utaingia mashakani, halikadhalika usaidizi wa mlo wenye virutubisho kwa watoto Laki Moja na Elfu themanini wenye utapiamlo.

Nchini DRC mtoto mmoja kati ya watoto kumi wanakabiliwa na utapiamlo huku watu milioni 6.3 wakiwa wanahitaji msaada wa chakula.