Watoto nchini Syria kuathiriwa na baridi kali:UNICEF

3 Disemba 2013

Wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likifanya mashauriano kuhusu mustakabali wa amani ya Syria, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema kiasi cha watoto milioni 5.5 wa Syria wanatazamia kutumbukia kwenye adha nyingine wakati kipindi cha msimu wa baridi kitapoanza hatua ambayo inatazamia kuwaweka kwenye hatari kubwa juu ya afya zao. George Njogopa na taarifa zaidi

UNICEF inasema kuwa mamilioni ya watoto walioko mtawanyikoni wanakabiliwa na ugumu wa maisha ikiwemo ukosefu wa sehemu rasmi za kujihifadhi.

Baadhiyaowako kwenye mazingira hatarishi na magumukamavile kuishi katika maeneo ambayo yanakumbwa na hali ya hewa inayobadilika mara kwa mara ikiwemo mvua na kuanguka kwa barafu.

Wasiwasi uliopo ni kwamba watoto walio chini ya umri wa miaka mitano wako hatarini zaidi kukubwa na magonjwa ikiwemo yale yanayohusisha na tatizo la kupumua tatizo ambalo limekua likisambaa kwa kasi kwenye eneohilo.

Kulingana na takwimu za UNICEF kiasi cha watoto milioni 4 wako mtawanyikoni nchini Syria pekee na kiasi kingine cha milioni 1.2 wanakutikana katika maeneo mengine ikiwemo kambi za wakimbizi, kuhifadhiwa kwa familia wenyeji katika nchi za jirani.

Afisa wa UNICEF Marixie Mercado anasema kuwa kumeanza kusambazwa huduma muhimu haza zile zinaweza kutoa msaada wakati wa msimu wa baridi.

 ( SAUTI YA MARIXIE MERCADO

Tangu mapema mwezi Oktoba UNICEF imekuwa ikijitahidi kuwapatia watoto vifaa vya kujikinga na baridi, kama vile nguo na  mablanketi, ambavyo vinasambazwa sambamba na mahema yanayofaa wakati wa msimu huu,  pamoja na nishati ya mafuta kuwezesha madarasa kuwa na joto. UNICEF pia inaweka akiba ya nishati ya mafuta kwenye maeneo ambayo si rahisi kufikika ili yaweze kupelekwa wakati wowote. Halikadhalika inaimarisha mifumo ya majitaka na kusafisha matenki ya maji bila kusahau kujenga misingi thabiti ya mahema yanayotumiwa na familia na katika kambi kwenye ukanda mzima."