Watu zaidi ya 15,000 wanahitaji misaada ya dharura Niger:OCHA

3 Disemba 2013

Zaidi ya watu 15,000 wapo katika hali mbaya Kusin Mashariki mwaNigerna kwamba misaada ya dharura inahitajika ili kunusuru maishayaokufuatia mafuriko makubwa yaliyosababishwa na kubasuka kwa kingo za  mto Komadougou .

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya usamaria mwema OCHA limesema kuwa mafuriko hayo yalianza kujitokeza katika kipindi cha miezi michache iliyopita na kuathiri sehemu kubwa ya eneohilo.

Kiwango cha maji kiliongezeka katika hali isiyotarajiwa katikati ya mwezi uliopita na kuzidisha maafa zaidi. Kulingana na timu ya wafanyakazi wa huduma za dharura mamia ya watu wanahitaji misaada wa chakula, maji yaliyotiwa dawa na huduma nyingine za afya. Jens Learke  ni msemaji wa OCHA

“Mafuriko pia yameathiri mfumo wa usafirishaji na kusababisha biashara ambayo ni tegemeo kuu la kipato kwa wakazi wa eneo hilo kudorora. Mamlaka za eneo hilo zinaripoti ongezeko la uingizaji wa vyakula kutoka Nigeria, lakini bei zimeongezeka mno. Mathalani bei ya kilo 100 ya unga imepanda kwa asilimia 30.”