Wagonjwa wengine watatu waliokumbwa na virusi (MERS-CoV) wagundulika Abu Dhabi

3 Disemba 2013

Shirika la afya ulimwenguni WHO limearifiwa juu ya kugundulika kwa wagonjwa wengine watatu wenye matatizo ya virusi vya (MERS-CoV) katika eneo la Mashariki baada ya uchunguzi wa kimaabara kukamilika.

Wagonjwa hao watatu ni kutoka familia moja iliyoko Abu Dhabi ambao ni mama mwenye umri wa miaka 32, baba mwenye wa miaka 38 na mtoto wa kiume ambaye taarifa zinasema kuwa ana umri wa miaka 8.

Wawili kati yao wako katika hali mbaya na wanaendelea kupata matibabu hospitalini.Taarifa zaidi zinasema kuwa familia hiyo haijawahi kusafiri nje na eneo wanaloishi na hawakumbuki kama wamewahi kukutana na mtu ambaye amewahi kukubwa na virusi hivyo.

WHO imezitaka nchi washirika wake kuchukua tahadhari ya mapema ikiwemo kutoa taarifa pindi wanaposhuku kuibuka kwa virusi vya ugonjwa huo