Mtaalamu wa haki za binadamu azuru Sri Lanka kutathimini hali ya wakimbizi wa ndani

2 Disemba 2013

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa kuhusu haki za binadamu Chaloka Beyani ameanza leo ziara ya siku tano nchini Sri Lankakutathimini hali jumla ya wakimbizi wa ndani nchini humo.

Amesema nia ni kwenda kukusanya taarifa kutoka pande zote zikiwemo za wakimbizi wa ndani na jamii zilizoathirika  hasa mjiniColombo,Jaffnana Mullaitivu.

Bwana Beyani pia ataangazia changamoto na fursa za suluhu ya wakimbizi wa ndani huku akijadili hatua zilizopigwa hasa katika kuwalinda na kuwapa msaada.

Kuanzia leo hadi Desemba 6 Bwana Beyani atakutana na wawakilishi wa serikali, jumuiya za kiraia na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa. Pia atazuru maeneo mbalimbali waliko wakimbizi wa ndani na kukutana nao na viongozi wao.

Bwana  Beyani anatarajiwa kutoa ripoti fupi baada ya ziara yake  na ripoti kamili itawasilishwa kwenye baraza la haki za binadamu June 2014.