Ajira kwa wenye HIV siyo tu ni haki bali pia ni tiba: ILO

Ajira kwa wenye HIV siyo tu ni haki bali pia ni tiba: ILO

Leo ni siku ya Ukimwi duniani ambapo shirika la kazi duniani ILO linasema kuwa mtu anayeishi an virusi vya HIV vinavyosababisha Ukimwi ana nafasi kubwa zaidi ya kukabiliana na matumizi ya dawa za kupunguza makali ya Ukimwi kuliko yule asiye na ajira.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO Guy Rider, akinukuu ripoti ya shirikalakeiliyotolewasambamba na maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani, amesema mwenye ajira ana nafasi ya asilimia 39 zaidi kukabiliana na matumizi ya dawa hizo kwa kuwa ana uhakika wa kupata chakula bora na hata ana uhakika wa fedha wakati wa kipindi cha matibabu.

Bwana Ryder amesema mtu mwenye virusi vya Ukimwi ambaye ana uhakika wa kipato na hifadhi ya kijamii anaweza kuendelea na matumizi ya dawa kwa muda mrefu wa maisha yake na hivyo ujumbe wa mwaka huu ni dhahiri ya kwamba ajira siyo tu ni haki bali ni sehemu ya matibabu.

Mwezi Juni mwaka huu ILO ilianzisha kampeni ya ushauri nasaha na kupima virusi vya HIV sehemu za kazi kama njia mojawapo ya kuwawezesha wafanyakazi kufahamu haliyaoya kiafya na iwapo wana virusi wanapatiwa maelekezo ya jinsi ya kuanza tiba.

ILO inasema mpango huo unalenga kuwafikia wafanyakazi Milioni Tano. Umoja wa Mataifa unasema karibu nusu ya watu Milioni 35 duniani wanaoishi na virusi vya Ukimwi duniani hawajui iwapo wana virusi au la na wengi wao ni wafanyakazi.