Skip to main content

MINUSMA yalaani ghasia huko Kidal nchini Mali

MINUSMA yalaani ghasia huko Kidal nchini Mali

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kuweka utulivu nchiniMali, MINUSMA umeshutumu vikali ghasia za karibuni huko Kidal kaskazini mwa nchi hiyo na kutaka pande zote husika kujizuia. Ghasia hizo za Alhamisi zimetokea licha ya mpango wa ulinzi wa ujulikanao kama Serval ambao unaratibiwa kwa pamoja na serikali ya Mali na MINUSMA kwa  usaidizi wa Ufaransa.

Taarifa ya ujumbe huo  imesema kwa usaidizi wa Serval waliweza kusaidia kuwapeleka majeruhi watatu hadi Gao kwa ajili ya matibabu. Ghasia hizo ziliibuka kabla ya kuwasili huku Kidal kwa Waziri Mkuu Oumar Tatam Ly na ujumbe wa serikali. Tangu mapema mwaka jana,Maliimeshuhudia mapinduzi ya kijeshi, kuibuka kwa mapigano mara kwa mara kati ya serikali na waasi wa Tuareg na kushikiliwa kwa eneo la kaskazini na waislamu wenye msimamo mkali.

Mwezi Aprili mwaka huu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilipitish azimio la kuruhusu kikosi cha walinda amani 12,600 wa MINUSMA na kuwapatia mamlaka ya kutumia njia zote zinazohitajika kurejesha utulivu na kulinda raia.