Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wakimbizi kutoka Syria wanabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye: UNHCR

Watoto wakimbizi kutoka Syria wanabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye: UNHCR

Watoto wa wakimbizi walio nchini Lebanon na Jordan wanakabiliwa na wakati mgumu siku za baadaye huku wakiwa wanalazimika kufanya kazi kutafutia familia zao au wakiwa wanalazimishwa kujiunga na makundi yaliyojihami kwa mujibu wa  shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa.

Utafiti uliofanywa kwa watoto wa wakimbizi wa Syria kwenye nchi za Lebanon na Jordan unaoyesha kuwa wengi wanasumbuliwa kisaikolojia kutokana na atahri za vita wakijipata kwenye familia zilizosambaratika na kukosa  masomo.

Utafiti huo unaonyesha kuwa watoto wadogo walio na  umri wa miaka saba hufanya kazi kwa masaa mengi  kazi zenye malipo haba au pila malipo kabisa wakifanya kazi kwa mazingira hatari. Kamishina mkuu wa haki za binadamu Antonio Geterres anasema kuwa hatua za haraka zinahitajika kumaliza mzozo ulio nchini Syria la sivyo vizazi vichavyo vitaathirika pakubwa. Volker Turk ni mkurugenzi wa masuala ya  usalama wa kimataifa kwenye shirika la UNHCR

(SAUTI YA VOLKER TURK)

Ni ukweli kwamba kuahama kunaashiriak taabu zilizopo. Ni wasi kuwa inapokuja kwa masuala ya watoto, kuhama huwaathiri watoto zaidi, sio tu watoto wakimbizi , lakini kama  unaweza kuangalia familia zinazowahifadhi ni muhimu kuhakikisha kuwa suala hili haliathiri watoto kwenye familia zinazowahifadhi. Suala la kuwa na nyumba limeathiriwa na kuhama. Kutahitajika jitihada na usaidizi kwa familia zinazotoa hifadhi na nchi zinazowahifadhi kuhakisha kuwa mzigo zinazoubeba nchini hizi umetwaliwa.”

UNHCR inakadiria kuwa zaidi ya watoto wa Syria  milioni 1.1 wanaishi kwenye nchi majirani.