Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sudan Kusini yazidi kutekeleza hukumu ya kifo hata baada ya kutia sahihi makubaliano ya UM

Sudan Kusini yazidi kutekeleza hukumu ya kifo hata baada ya kutia sahihi makubaliano ya UM

Ofisi ya haki za bindamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa watu wanne wamenyongwa nchini Sudan Kusini huku wengine 200 wakiwa kwenye  orodha ya kusubiri kunyongwa. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)

Kulingana na ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa ni kuwa idara ya mahakama nchini Sudan Kusini inakabiliwa na wakati mgumu wa  kukabilina na idadi kubwa ya watu walio gerezani ambao  hawajapata huduma za mahakama. Watu 14 wamenyongwa tangu nchi hiyo kupata uhuru mwaka 2011 hata baada ya kutia sahihi  makubaliano ya Umoja wa Mataifa kuhusiana na hukumu ya kifo. Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa idadi ya wale wanaonyongwa  nchini  Sudan Kusini  huenda ikawa ni ya juu. Cécile Pouilly ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa.

(SAUTI YA CECILE POUILLY)

Wengi wa watu walio gerezani Sudan Kusini hawana uwakilishi wa kisheria au haki ya kupata uwakilishi wa kisheria bure. Kulingana na sheria ya kimataifa, hukumu ya kifo inatakiwa tu kutekelezwa baada ya hukumu inayotolewa na mahakama yenye uwezo mzuri wa kufanya hivyo, baada ya hatua zifaazo kisheria, pamoja na njia zote za kuhakikisha haki, ikiwemo uwakilishi wa kisheria na haki ya kuomba rufaa kwa mahakama ya juu zaidi.”