Idadi ya walioathirika na kimbunga Haiyan sasa ni zaidi ya milioni 14:OCHA

29 Novemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu OCHA linasema kuwa idadi ya watu walioathirika na kimbuka Haiyan nchini Ufilipino imezidi kupindukia.

Kwa mujibu wa OCHA, zaidi ya watu milioni 14.4 wameathiriwa na kimbunga hicho ambapo kati yao, milioni 3.62 wamekosa makazi, milioni 1.1 nyumba zao zimebomolewa na vifo vilivyoripotiwa hadi sasa vimefikia 5,500 huku wengine 1,157 hawajulikani waliko. Taarifa ya Grace Kaneiya inafafanua zaidi

(RIPOTI YA GRACE KANEIYA)

OCHA inasema kuwa kazi kubwa iliyoko mbele ni kujenge umpya nyumba za wale walioathirika na kimbunga hicho na kulingana na mazingira yalivyo kwa sasa ujenzi huu huenda ukakabiliwa na changamoto nyingi.

Kuna hali ya ukosefu wa vifaa muhimu vya ujenzi na baadhi ya maduka yamepandisha bei ya vifaa mara dufu kutokana na mahitaji makubwa yanayojitokeza.

Pia suala la upatikanaji wa chakula ni eneo jingine ambalo linaendelea kugonga vichwa vya habari na baadhi ya maeneo yamekosa kabisa chakula na mahitaji mengine muhimu ya kibinadamu. Kama anavyofafanua Vorrine Momal-Vanian.

(SAUTI YA MOMAL-VANIAN)