Vifo vya raia wa Haiti katika pwani ya Bahamas vitupe funzo:IOM

29 Novemba 2013

Vifo vya wazamiaji 30 wa Haiti waliokumbwa na umauti wakati wakiwa safarini katika ufukwe wa Bahama mapema wiki hii kumezidi kuongeza hali ya wasiwasi kuhusiana na wimbi la wahamiaji haramu wanaokwenda katika nchi za mbali huku wakitumia mashua zisizo na usalama.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa linalohusika na wahamiaji IOM, kuna hali ya kutia wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa matukio ya vifo vinavyosababishwa na usalama mdogo wa mashua. George Njogopa na ripoti kamili

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Shirika hilo la kimataifa linasema kuwa kujitokeza kwa vifo vya mara kwa mara katika maeneo ya Caribbean, Mediterranean,bahari ya Hindi pamoja na bahari Sham ni king’ora kinachoashiria ulazima wa kufanyika jambo juu ya matukio hayo.

Limesema kuwa lazima jumuiya ya kimataifa iamuke na kuanza kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha kwamba matukio ya namna hiyo hajajirudii tena.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo la kimataifa William Lacy amesema kuwa jamiii ya kimataifa inawajibu wa kuyatafutia ufumbuzi masuala ya uhamiaji ambayo ndiyo yanayosababisha vifo vya mara kwa mara.

Ametaja makundi ya watu wanaotumbukia kwenye uhamiaji huo ni pamoja na wale wanaomba hifadhi ya kijamii na kisiasa, wakimbizi na wale wanaokwenda nchi za ng’ambo kwa ajili ya kusaka maisha bora. Christiane Berthiume wa IOM anafafanua zaidi

(SAUTI YA CHRISTIANE BERTHIUME)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter