Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yaomba dola milioni 10 kuwarejesha Wasouth Sudan kwao

IOM yaomba dola milioni 10 kuwarejesha Wasouth Sudan kwao

Shirika la Kimataifa la uhamiaji IOM linaomba dola milioni 10.5 ili liweze kutoa msaada wa dharura wa kuwarejesha watu wasiojiweza wa Sudan Kusini kwao. Watu hao wamekwama mjini Khartoum Sudan kwa muda sasa. IOM inasema watu hao hawana uwezo na njia yoyote ya kuwarejesha nyumbani Sudan Kusini.

Shirika hilo limeongeza kuwa watu hao wamekuwa wakiishi kwenye makazi ya muda  wakiwa hawana huduma muhimu kama za afya, usafi , maji na huduma zingine na hivyo ni muhimu saana wakarejeshwa nyumbani ambako wanaweza kupata huduma hizo.