Masaibu ya wakimbizi wa Syria walioko Lebanon yaangaziwa

27 Novemba 2013

Siku chache baada ya Umoja wa Mataifa kutangaza tarehe 22 January mwakani ya kufanyika kwa mkutano wa pili wa amani kuhusu Syria huko Geneva, wakimbizi wa nchi hiyo walioko katika kambi nchini Lebanon wanaelezea madhila wanayokutana nayo.

Hapa katika mji wa Arsal nchiniLebanonkuna foleni kubwa ya watu nje ya kituo cha usajili. Zaidi ya familia 60 wamepata makazi katika msikiti akiwamo Muhamed kutokaHomshuku wengine wakiwa katika  chumba cha harusi aliyefika hapa siku mbili zilizopita na mke wake na mtoto. Familia hii imehama karibu mara tano sasa tangu mzozo huu ulipoanza.

 SAUTI YA MOHAMED

Tuko familia 15 tunaishi wote pamoja lakini kuna familia 65 katika jrngo nzima. Tunalala sakafuni bila chochote. Watoto wanahitaji maziwa, chakula lakina hatuna. Tulioondoka Qarra na nguo tulizovaa pekee. Hatukuweza kubeba chkula, nguo au mablanketi.”

UNHCR na washirika na Serikali wanafanya kazi pamoja kuhifadhi idadi hii kubwa ya wakimbizi.

Maeve Murphy ni msimamizi kutoka UNHCR

 “Karibu siku mbili zilizopita ghasia zilizuka Qarah. Kufuatia mapigano hayo baadhi ya familia hawakuwa na namna wakalazimika kuhamia Arsal. Kwa hivyo tumeleta pamoja baadhi ya mashirika kutoa msaada kwa karibu familia 1,000 ambazo zimefika kwa kipindi cha siku mbili zilizopita. Ijapokuwa familia zingine ziko safarini tumeweza kufika maeneo mengine nchini Lebanon na Syria. Tunajaribu kushughulikia mahitaji yaliyopa Arsal kwa sasa kwa usambaazji wa mahitajiya  msingi yanayohitajika.”

Kwa sasa Mohamed amepata usalama lakini ana pesa za kulisha familia kwa siku chache tu. Na hajui namna ya kupata kazi Lebanon.