Ban na Kim wazungumzia nishati endelevu

27 Novemba 2013

Ilikufanikisha malengo ya nishati endelevu kwa wote ni muhimu kukuza uwekezaji mkuu na wa ziada amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon

Akiwa ameambatana na rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim katika mkutano na waandishi wa habari mjini New York kufuatia kikao cha ngazi ya juu cha bodi ya mpango wa nishati endelevu katibu mkuu Ban amesema nishati endelevu ni kwa ajili ya kupunguza umaskini na kuibua fursa ili kupambana na mabadiliko ya tabia nchi.

 Amesema kufanya hivyo ni kuweka msingi kwa mustakabali ambao dunia inauihitaji na kuongeza

 (Sauti ya Ban)

 "Nishati endelevu ni uzi wa dhahabu unaounganisha maendeleo ya kiuchumi, uswa wa kijamii, halia ya hewa thabiti na mazingira boa. Tunahitaji kuweka huduma za kisasa za nishati kwa wote. Lakini yatupasa  kufanya kwa uendelevu"