Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya jitihada China yahiizwa kuhifadhi mazingira:UNEP

Licha ya jitihada China yahiizwa kuhifadhi mazingira:UNEP

Licha ya juhudi za China za kukuza uchumi unaolinda na kuhifadhi mazingira taifa hilo bado linakabiliwa na changamoto za kimazingira na kijamii ambazo lazima zishughulikiwe iwapo nchi hiyo inalenga kwa dhati kutimiza malengo endelevu ya maendeleo.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa wiki hii na wizara ya uhifadhi wa mazingira nchini China, MEP, na shirika la Umoja wa Mataifa la mazinginra UNEP. Ripoti hiyo ambayo imepewa jina Safari ndefu ya China ya kuhifadhi mazingira imeangazia uhuishaji wa nishati, viwanda vya mazingira na sekta ya saruji.

Ripoti hiyo hiyo pia inabainisha kuwa taifa hilo ndilo linaloongoza duniani kwa uwekezaji wa uhuishaji wa teknolojia ya nishati na viwanda.