Serikali ziweke mipango ya maendeleo ya kupunguza majanga:ESCAP

27 Novemba 2013

Kujenga uwezo mkubwa wa kukabiliana na majanga katika eneo la Asia-Pacifiki ndio ajenda kuu kwenye mkutano wa siku tatu ulioanza Jumatano katika tume ya Umoja wa Mataifa ya kiuchumi na kijamii kwa nchi zaAsiana Pacific ESCAP.Taarifa ya Flora Nducha inaarifu

 (TAARIFA YA FLORA NDUCHA)

 Mkutano huo unaofanyika mjini Bangkok Thailand umewaleta pamoja maafisa wa serikali kutoka nchi zaidi ya 25. Janga la kimbunga Haiyan ni moja ya mifano ya karibuni ya zahma zilizokumba Asia-Pacific katika miaka michache iliyopita, na inadhihirisha umuhimu wa haja ya kuwa na mtazamo imara wa kujenga uwezo kwa nchi hizo wa kukabili na kujikwamua baada ya kukumbwa na majanga ya asili.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Ufilipino kwenye ESCAP Bi Jocelyn S. Batoon-Garcia athari za kimbunga Haiyan zinadhihirisha haja ya haraka ya kubadili mtazamo na kuwa mipango ya hatua za kijamii , kikanda na kitaifa ili kudhibiti na kujikwamua baada ya kukumbwa na majanga.