Global Fund yapigwa jeki kwa dola milioni 46 kupitia uuzaji wa mnada

27 Novemba 2013

Mfuko wa Global Fund kwa ajili ya kupambana na malaria, kifua kikuu na HIV umepigwa jeki kwa mchango wa dola milioni 46, zilizotokana na zoezi la uuzaji wa mnada lililoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Renew, Energize and Donate (RED), pamoja na michango mingine. Joshua Mmali na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JOSHUA)

Zoezi hilo la uuzaji wa mnada liliandaliwa na shirika la RED mnamo Novemba 23, 2013 mjini New York, na likashirikisha nyota wengi katika sekta ya utumbuizaji kama vile mwanamuziki Bono na wasanii wengine.

Bidhaa za sanaa zilizoundwa na Sir Jonathan Ive na Marc Newson ziliuzwa kwa mnada, na kuchangisha dola milioni 13, ambazo hazina ya Bill na Melinda Gates ilijumlisha na kufikisha dola milioni 26. Dola milioni 20 zaidi zilitoka Marekani na Uingereza.

Mkurugezni Mkuu wa Global Fund, Mark Dybul, alilishukuru shirika la RED na wasanii waloshiriki kwa ubunifu wao na kuchagiza uchagishaji wa rasilmali za kupambana na virusi vya HIV.