Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yapitisha idadi ya wakimbizi wa Ivory Coast iliowarudisha nyumbani kutoka Liberia

UNHCR yapitisha idadi ya wakimbizi wa Ivory Coast iliowarudisha nyumbani kutoka Liberia

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR  Iemepitisha idadi ya wakimbizi  wa Ivory Coast lililowarudisha nyumbani kwa hiari kutoka  nchini Liberia ikiwa pia na mipango ya kuwarudisha  nyumbani wakimbizi zaidi kabla ya mwisho wa mwaka huu. Jason Nyakundi na ripoti kamili.(Taarifa ya Jason)

Hadi mwishoni mwa juma lililopita UNHCR ilikuwa imewasaidai wakimbizi 16,232 kurudi nyumbani kwenda kwa meno ya magharibi mwa Ivory Coast. Idadi ya wakimbizi waliorudi nyumbani mwaka 2013 ni mara mbili zaidi  ya idadi  ya ya wakimbizi waliorudi nyumbani mwaka 2012 na 2011.

 Mjumbe wa UNHCR nchini Liberia Khassim Diagne  amesema kuwa kwa ushirikiano na serikali ya Liberia wametimiza lengo lao akiongeza kuwa idadi ya wakimbizi wanaorudi nyumbani itazidi kuongezeka.

Hali ya usalama kati ya mpaka wa Liberia na Ivory Coast  imekuwa yenye changamoto kubwa kwenye mpango huo uliozinduliwa na UNHCR  mwaka 2011. Diagne amesema kuwa kuboreshwa kwa usalama kulichagia pakubwa kufanikiwa kwa shughuli hiyo huku mashua zlizotumiwa kwenye mto Cestos zikiwa mbadala wa barabra zilizofurika