Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpatanishi wa Darfur akutana na rais wa Chad

Mpatanishi wa Darfur akutana na rais wa Chad

Kiongozi wa ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa mzozo wa Darfur nchini Sudan Mohamed Ibn Chambas amekutana na Rais wa Chad Idriss Derby katika kile kinachoelezwa kwamba ni jaribio la kidiplomasia la kufanikisha mazungumzo ya amani ya Darfur.

Msuluhishi huyo wa kimataifa anayeongoza UNAMID ametoa picha halisi ya usalama katika jimbo la Darfur wakati alipomwelezea rais Derby hatua zinazopigwa juu ya utanzuaji wa mzozo huo uliodumu kwa muda sasa.

Ziara yake hiyo mjini N’Djamena inakuja ikiwa imepita siku chache tu tangu vikosi vya kulinda amani kutoka Rwanda kuvamiwa na askari wake mmoja kuuliwa na watu wasiojulikana.

Kwa upande wake rais Derby alizingatia umuhimu wa kupatikana amani ya kudumu , akisema kuwa suluhu itayopatikana katika jimbo hilo itatoa mustakabali mwema kwa eneo nzima.