Baraza Kuu lapitisha maazimio ya kuunga mkono Palestina na suala la Golan

26 Novemba 2013

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Wanachama wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, leo wamepiga kura kuhusu maazimio matano tofauti yanayounga mkono Palestina, pamoja na jingine kuhusu suala la eneo la Golan nchini Syria.

Matukio hayo katika ukumbi wa Baraza Kuu yametokea siku chache kabla ya kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kusimama bega kwa bega na watu wa Palestina, ambayo ni Novemba 29.

Maazimio hayo yote yameungwa mkono kwa wingi wa kura, huku yakipingwa kwa wastani na wanachama 6 pekee, na wengine wakiwa hawapendelei upande wowote.

Akitoa shukrani zake kwa uungwaji mkono huo, Mwangalizi wa Palestina kwa Umoja wa Mataifa amesema

"Ningependa pia kuzishukuru nchi zote ambazo zimepiga kura za kuunga mkono. Tunashukuru sana kwa kura hizo kwa maazimio haya yote. Kwetu sisi, jamii ya kimataifa, busara yake, na ulinzi wake wa sheria ya kimataifa, ni chanzo cha matumaini kwa watu wa Palestina kuendeleza juhudi za kutimiza haki zetu za kimsingi za kitaifa " .

Azimio la kwanza linahusu kuweka kamati kuhusu utekelezaji wa haki za kimsingi za watu wa Palestina, la pili linahusu haki za Palestina kwenye sekritariati ya Umoja wa Mataifa, la tatu linahusu kuzingida programu maalumu kwenye idara ya habari na mawasiliano kwenye sekritariati ya Umoja wa Mataifa kuhusu suala la Palestina, la nne likihusu utatuaji wa suala la Palestina kwa njia ya amani na la tano likuhusu mji wa Jerusalem.

Mwakilishi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa, alikuwa na haya ya kusema

"Maazimio haya yanatimiza tu uwekaji taasisi nyingine zenye mizigo zaidi, utataribu wenye ukiritimba zaidi na wenye na utaratibu wa kuharibu fedha. Nchi nyingi zinakabiliana na hali ngumu kiuchumi nyumbani, na uchumi wa kimataifa unakabiliwa na shinikizo kubwa. Lakini Wapalestina wanamudu kuweka shinikizo kwa mataifa mengi katika ukumbi huu kutenga rasilmali zenye thamani kwa idara za Umoja wa Mataifa zinazodhalilisha Israel.”

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter