Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA kuhifadhi kidigital kumbukumbu za wakimbizi wa Kipalestina

UNRWA kuhifadhi kidigital kumbukumbu za wakimbizi wa Kipalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limezindua sehemu ya kwanza ya mfumo mpya wa kumbukumbu kwa njia ya digital ambao unajumuisha zaidi ya nusu ya negative za picha, machapisho, slides, filamu na kaseti za video ambazo zinakumbukumbu za Nyanja zote za maisha na historia ya wakimbizi wa Kipalestina tangu mwaka 1948 hadi sasa.

Kundi la kwanza la kumbukumbu za picha na filamu ni sehemu ya maonyesho yaitwayo “safari ndefu” yaliyoanza leo kituo cha Al-Ma’mel , mji mkongwe wa Jerusalem.

Makumbusho hayo yameorodheshwa na shirika la Umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO kwenye “kumbukumbu ya dunia” ambayo inajumuisha makusanyo ya utamaduni na historia za muhimu.