Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yafanya kampeni dhidi ya ukatili wa kingono kambi za wakimbizi Uganda

UNHCR yafanya kampeni dhidi ya ukatili wa kingono kambi za wakimbizi Uganda

Shirika la Umoja wa Mataifa Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huko Hoima nchini Uganda limeanza kampeni ya siku kumi na sita za kupinga unyanyashaji wa kingono na mizozo ya kijinsia kwenye kambi za wakimbizi ya Kyangwali na Kiryandongo. John Kibego wa redio washirika ya Spice FM ana ripoti kamili kutoka Uganda.

(Tarifa ya John Kibego)

Kampeni hii imaendeshwa kwa kauli mbiu: Usalama shuleni: Waalimu na wanafunzi mushirikiane kutokomeza unyanyashaji wa kingono na mizozo ya kijinsia shuleni.

Katika kipindi cha siku kumi na sita, watakuwa na madhimisho ya siku ya ukimui duniani tarehe mosi Disemba, siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu tarehe tatu, na tarehe sita waadhimishe siku ya mauaji ya wanawake 14 waliouawa wakitetea haki za wanawake kwenye chuo kikuu cha Montreal Canada mwaka 1989.

Wataafika kilele tarehe kumi kwa kwadhimisha siku ya haki za binaadamu duniani kama anavyoeleza Johansen Kasenene afisa wa huduma za jamii kweny kutoka ofisi ya UNHCR ya Hoima.

(Sauti ya Bi. Kasenene)