Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya uhaba wa kawi Gaza:UM

Hatua za dharura zichukuliwe dhidi ya uhaba wa kawi Gaza:UM

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa Richard Falk ametaka kuchukuliwa kwa hatua za dharura kukabilina na uhaba wa kawi kwenye utawala wa Palestina hali ambayo imewaacha watu milioni 1.7 kwenye  ukanda wa Gaza kwenye hali ya kutatanisha.

Kwa kipindi cha majuma matatu sasa tangu kituo cha kuzalisha kawi kufungwa kutokana na uhaba wa mafuta masaa ya kupata kawi yamepunguzwa hadi  sita kwa siku.

Mjumbe huyo ambaye ametwikwa jukumu la kufuatilia hali ya haki za bindamu kwenye utawala wa Palestina na baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameonya kuwa hali ilyo sasa huenda ikawa mbaya zaidi. Mjumbe huyo amesema kuwa uhaba huo wa mafuta na kawi umesababisha madhara makubwa  na kuvuruga utoaji wa huduma muhimu kama afya , maji na usafi. Chini ya nusu na mahitaji yote ya kawi yanaafikiwa na kuvuruwa kwa huduma za afya zikiwemo za upasuaji, hifadhi za damu na huduma za wagonjwa mahututi vinaweka hatarini maisha ya wagonjwa wengi.

Kwa kipindi cha majuma mawili karibu wanyeji 3000 wakiwemo watoto wanoishi kwenye eneo la  Az Zeitoum wamekuwa wakihangaishwa na maji taka yaliyo mitaani baaada kutuo ya kuoshea maji hayo kukumbwa na uhaba wa kawi.