Waomba hifadhi kisiwa cha Pacific wanakabiliwa na mateso:UNHCR

26 Novemba 2013

Ripoti mbili zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR zimebaini kuwa mamia ya watu walioomba hifadhi nchini Australia na kisha kuhamishia katika visiwa vya Nauru na Manus vilivyoko huko Papua New Guinea wanaishi  katika maisha ya mateso na hali ya kukatisha tamaaa. Taarifa zadi na George Njogopa.

(TAARIFA YA GEORGE)

Katika utafiti wake huo UNHCR imesema inatambua hatua zinazochukuliwa na serikali ya Australia ambayo imedhamiria kukabiliana na wimbi la biashara haramu ya watu wanaosafiri kwa njia ya magendo, lakini wakati inatekeleza mikakati yake hiyo lazima itambue wajibu wa kuwalinda raia kwa kuwapa uhuru, haki na kuheshimu utu wao.

Ripoti pia imesema kuwa mamia ya raia wanaoingia nchini humo kwa ajili ya kuomba hifadhi wanaandamwa na matukio ya kusikitisha na wakati mwingine hutumbukia kwenye matatizo makubwa.

Baadhi yao wanatiwa korokoroni huku wakikosa fursa zinazotambuliwa na sheria za kimataifa

Pia imetaja hali mbaya inayokutikana katika visiwa vyote vilivyoko Papua New Guinea ambavyo hutumika kuwahifadhi raia wanaoomba hifadhi wakati makaratasi yao yakiendelea kushughulikiwa.

Kwa upande mwingine,ripoti hiyo imeashiria kupatikana kwa ufumbuzi wa kudumu lakini imezitaka mamlaka zinazohusika kuzifanyia marekebisho baadhi ya sera zake ambazo zinadaiwa kukandamiza uhuru wa waomba hifadhi. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR

(SAUTI YA ADRIAN EDWARD)

 

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud