Tunataka lengo mahsusi kwa wanawake kwenye ajenda endelevu: UNWomen

25 Novemba 2013

Mkuu wa shirika la linalohusika na masuala ya wanawake kwenye Umoja wa Mataifa Phumzile Mlambo-Ngcuka ametaka kuwepo kwa lengo mahsusi kuhusu wanawake kwenye ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015 kama njia mojawapo ya kuhakikisha kuwa masuala ya ulinzi na maendeleo kwa kundi hilo yanapatiwa mkazo.

Ametoa kauli hiyo mjini New York wakati wa hafla maalum ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake hafla ambayo ilikuwa na rangi maalum…

Bi Mlammbo-Ngcuka akaweka bayana kuwa wametupia kitu cha machungwa kama sehemu ya vazi ili kuonyesha mshikamano na wasichana na wanawake wanaokumbwa na madhila mbali mbali ikiwemo..

(Sauti ya Phumzile)

"Tunashikamana na wanawake wanaouawa kwa sababu tu wanawake, wanawake wahanga wa manyanyaso ya kwenye mtandao, wanawake wanaobakwa vyuoni, wakati wao ni mchango muhimu kwa jamii, lakini uhalifu huo unafanyika huko. Wanawake wanaonyanyaswa sehemu za umma, sasa tunashikamana na wanawake na wasichaan wanaonyanyaswa kabla, wakati na baada ya mizozo. Na sasa tumepitisha maazimio kusaidia wanawake hawa kwa hatua ambazo ni bora zaidi kuliko awali.”

Hatimaye kiashirio hicho kikawa ni cha simulizi kuhusu madhila yanayokumba wanawake kuanzia vipigo majumbani….. , ndoa za umri mdogo… na hadi kule Mexico kwenye mji wa Suarez ambako ilielezwa kuwa idadi ya wanawake na watoto wa kike inapungua kila siku kutokana na ukatili.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud