Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban asikitishwa na shambulio lingine Darfur

Ban asikitishwa na shambulio lingine Darfur

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema amesikitishwa sana kubaini kulikuwa na shmabulio lingine lililofanywa na mtu mwenye silaha dhidi ya msafara wa vikosi vya pamoja vya kulinda amani Darfur vya Umoja wa Mataifa na Muungano wa Afrika UNAMID karibu na Kabkabiya Darfur Kaskazini.

Katika shambulio hilo mlinda amani mmoja kutoka Rwanda ameuawa. Ban ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya mlinda amani huyo na serikali ya Rwanda.

Katibu Mkuu amelaani vikali shambulio hilo dhidi ya UNAMID na anatarajia serikali ya Sudan kuchukua hatua ya kuwafikisha kwenye mkono wa sheria waliotekeleza shambulio hilo na mashambulio yaliyopita.