Vijana barubaru hawapati huduma wanazohitaji dhidi ya Ukimwi:WHO

25 Novemba 2013

Zaidi ya vijana milioni mbili walio kati ya umri wa miaka 10 na 19 wanaoishi na virusi vya ugonjwa wa ukimwi hawapati usaidizi wanaohitaji kuwawezesha kuwa na afya na katika kuzuia maambukizi mapya kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO. Jason Nyakundi na taarifa kamili.

(TAARIFA YA JASON NYAKUNDI)

WHO inasema kuwa kushindwa kuwapa huduma vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi kumechangia kwa asilimia 50 vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa ukimwi .

Kabla ya maaadhimisho ya siku ya ukimiwi duniani ambayo yatafanyika tarehe mosi mwezi Disemba WHO imetoa mipangilio mipya ya kuwapima na kuwashauri vijana wanaoishi na virusi vya ukimwi amboyo ndiyo ya kwanza inayowalenga vijana wakiwemo wanoishi na virusi vya ukimwi na wale walio kwenye hatari ya kuambukizwa.

Kati ya hatua ambazo WHO ingependa zitekelezwe ni pamoja kufanyiwa mabadiliko sheria ambazo zitarahizisha huduma zinazotolewa kwa vijana.

Dr Gottfriend Hirnschall ni mkurugenzi kwenye idara ya ukimwi kwenye shirika la WHO.

(SAUTI YA DR GOTTFRIED) ANDIKA TUTASOMA HUKU

“Kuna maambukizi makubwa hasa miongoni mwa vijana kutoka kwa kile tunachokitaja kuwa watu wengi. Hawa ni vijana wa kike walio kusini mwa jangwa la sahara. Vijana wa kiume wanaofanya ngono na wanaume, Tumeona visa hivi kwenye miji mingi ya Asia, Bangladesh, Kuala Lumpur na Jakarta. Vijana wanaojidunga madawa kwa mfano mashariki mwa Ulaya tunajua ya kwamba zaidi ya asilimia 30 ya watumiaji madawa ya kulefya wana virusi vya ukimwi na pia pia vijana walio kwenye hatari ya kudhulumiwa kimapenzi. Lazima tuwahudumie kwa njia nzuri vijana . Ni lazima tutoe huduma zilizo bora, tuweze kuwafikia vijana. Na ni lazima tuhakikishe kuwa huduma zinazotolewa kwa watu wazima pia zinatumiwa kwa vijana ikiwemo kuwepo kwa vifaa bora vya kupima na kutibu na kadhalika.”

Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF linasema kuwa moja kati ya visa saba vipya vya maambukizi ya virusi vya ukimwi viko miongoni mwa vijana.