Ukiukwaji wa haki za binadamu Eritrea wasababisha maelfu kukimbilia uhamishoni

25 Novemba 2013

Kiasi cha raia 3,000 wa Eritrea wanaripotiwa kuondoka nchini mwao kila mwezi ili kujiepusha na mienendo ya uvunjifu wa haki za binadamu unaodaiwa kufanywa na serikali pamoja na vyombo vya usalama. Taarifa hiyo imeibuliwa na Wataalamu huru wa shirika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa. George Njogopa na taarifa kamili.

(Taarifa ya George)

Mtaalamu huru wa Umoja a Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu nchini Eritrea Sheila Keetharuth, amebainisha madhira wanayokumbana nayo raia wa nchi ikiwemo yale ya kuteswa na vyombo vya dola.

Vikosi vya serikali pamoja na taasisi za kiusalama zinadaiwa kutumia mbinu za kiuchumi kuwabinya wananchi wengi ambao kutokana na kuzingirwa na maisha magumu wamelazimika kukimbilia nchi za mbali wakitumia njia hatarishi ambazo baadhi yake zinaweka reheni maisha yao.

Bi Keetharuth ambaye amekuwa akiitembelea nchi hiyo pamoja na nchi nyingine za Tunisia na Malta anasema kuwa raia wa Eritrea wanaandamwa na vitisho vikali vya kuteswa na kushurutishwa.

Kutokana na hali hiyo, mtaalamu huyo ameitaka serikali ya Eritrea kuwajibika mara moja kwa kuhakikusha kwamba mwenendo huo unakomeshwa na wahusika wa matukio hayo kuchukuliwa hatua