Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukatili dhidi ya wanawake ni moja ya ukiukwaji mkubwa wa haki a binadamu: Rais wa Baraza Kuu

Ukatili dhidi ya wanawake ni moja ya ukiukwaji mkubwa wa haki a binadamu: Rais wa Baraza Kuu

Siku kumi na sita za Maadhimisho ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana zianaanza leo, ambapo dunia inahamasishwa kupinga vitendo hivyo. Joseph Msami amefuatilia tukiohilona  hii ni taarifa yake

(TAARIFA YA MSAMI)

Akitoa ujumbe wake katika kuanza kwa siku Kumi na Sita za kupinga ukatili dhidi ya wanawake na wasichana  Rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa John Ash amesema ukatili ikiwa pamoja na ule wa kingono ndiyo mbaya na umeenea zaidi na unaokiuka haki za wanawake.

Amesema ukatili huo unaathiri wanawake na wasichana hata kabla ya kuzaliwa kwao na kuendelea katika maishayaoyote na hutekelezwa na wanafamilia, wageni na jamii kwa ujumla.

Nchini Tanzani mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanwake na wasichana umelisukuma jeshi la polisi kuanzisha dawati maalum la kushughulikia vitendo hivyokamaanavyofafanua kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Ilala Marietta Minanji

(Sauti Minanji)