Muafaka wa mipango ya nyuklia ya Iran wakaribishwa na Katibu Mkuu

25 Novemba 2013

Muafaka wa muda kuhusu mipango ya nyuklia ya Iran uliotangazwa Jumapili umekaribishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.

Kwa mujibu wa ripoti wawakilishi wa Marekani, Uingereza, Urusi, Uchina, Ufaransa na Ujerumani ambao hujulikana kama P5+1 wamefikia makubaliano naIranmapema Jumapili.

Iran imearifiwa kukubali kusitisha baadhi ya mipango yake ya nyuklia kwa malipo ya kulegezwa baadhi ya vikwazo ilivyowekewa nchi hiyo kutokana na shuku kwamba ina mipango ya kuunda silaha za nyuklia.

Katika taarifa yake Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban amepongeza majadaliano hayo kwa hatua yaliyofikia. Taarifa iliyoolewa inasema “Mkataba wa miezi sita unaweza kuwa ndio mwanzo wa makubaliano ya kihistoria kwa watu na mataifa ya Mashariki ya Kati na kwingineko”

Bwana Ban amezitaka nchi zinazohusika kufanya kila linalowezekana kuendelea hatua hizo za kutima matumaini  na kuendeleza majadiliano kupanua wigo wa muafaka huo.

Ban ameitaka pia jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mchakato huu ambao endapo utaruhusiwa kufanuikiwa basi utakuwa na faida ya muda mrefu kwa pande zote .

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter