Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya chanjo kwa watoto Ufilipino kuanza Jumatatu: OCHA

Kampeni ya chanjo kwa watoto Ufilipino kuanza Jumatatu: OCHA

Normal

0

false

false

false

MicrosoftInternetExplorer4

st1\:*{behavior:url(#ieooui) }

/* Style Definitions */

table.MsoNormalTable

{mso-style-name:"Table Normal";

mso-tstyle-rowband-size:0;

mso-tstyle-colband-size:0;

mso-style-noshow:yes;

mso-style-parent:"";

mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;

mso-para-margin:0in;

mso-para-margin-bottom:.0001pt;

mso-pagination:widow-orphan;

font-size:10.0pt;

font-family:"Times New Roman";

mso-ansi-language:#0400;

mso-fareast-language:#0400;

mso-bidi-language:#0400;}

Hivyo ndivyo Mkuu wa ofisi ya masuala ya usaidizi wa kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, Valerie Amos alipoanza mkutano wake na waandishi wa habari mjini New York, akieleza kile alichoshuhudia huko Ufilipino baada ya kimbunga Haiyan kupiga nchi hiyo na kusababisha vifo na majeruhi pamoja na kupoteza makazi.

Bi. Amos ambaye amekwenda Ufilipino mara mbili baada ya kimbunga hicho amesema janga ni kubwa na licha ya kwamba nchi hiyo huwa na maandalizi makubwa dhidi ya majanga, lakini lililotokea ni janga kubwa linalohitaji usaidizi wa kimataifa.

Amesema huduma za msingi kama vile maji safi, afya na benki zilikatika lakini sasa zimerejea hususan huko Tacloban lakini bado watu wana hofu kwani msimu wa vimbunga bado haujamalizika. Halikadhalika amezungumzia chanjo kwa watoto dhidi ya magonjwa.

  “Kampeni ya chanjo kwa watoto nusu Milioni walio na umri wa chini ya miaka mitano dhidi ya Surua na Polio pamoja na matone ya Vitamini A itaanza Jumatatu.”

 Mkuu huyo wa OCHA akaulizwa swali kuhusu usaidizi unaoendelea na ombi la awali la dola Milioni 301iwapo linatosha..

 “Ombi la awali lilikuwa dola Milioni 301 na hadi sasa tumepata asilimia 40 tu tunatarajia ombi litaongezeka kwani kuna jamii ambazo hatujafikia, tutafanya tathjmini mpya ya ombi wiki ya kwanza ya mwezi Disemba, tayari tuna timu ziko huko na utakubali kuwa kufanya tathmini siku za mwanzoni kabisa mwa janga hilo haikuwa muafaka.”

 Bi. Amos amesema takwimu mpya kutoka serikali ya Ufilipino zinasema hadi sasa watu zaidi ya Elfu Tano Mia mbili wamekufa kutokana na kimbunga hicho na bado wanaendelea kuthibitisha taarifa za vifo na watu waliopotea kwenye maeneo mengine.