Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wigo wa vyanzo vya ajira upanuliwe: Dkt. Kituyi

Wigo wa vyanzo vya ajira upanuliwe: Dkt. Kituyi

 

Wiki hii Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo, UNCTAD limetoa ripoti kuhusu nchi zenye maendeleo duniani, LDCs kauli mbiu ikiwa  ustawi na ajira kwa maendeleo jumuishi na endelevu. Nchi hizo ziko 48 na miongoni mwao 34 zinatoka Afrika ikiwemo Burundi, Rwanda, Uganda na Tanzania. Je ni mambo yapi yameangaziwa? Nini majaliwa ya nchi hizo? Patrick Maigua wa Radio ya Umoja wa Mataifa, Geneva, Uswisi alifanya mahojiano na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dokta Mukhisa Kituyi na hapa Mkuu huyo wa UCTAD anaanza kwa kuzungumzia yaliyojiri kwenye ripoti hiyo.