Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wahamiaji wasio na vibali wakwama mipakani huko Maziwa makuu; IOM yatoa usaidizi

Wahamiaji wasio na vibali wakwama mipakani huko Maziwa makuu; IOM yatoa usaidizi

Wakati idadi kubwa ya wahamiaji wasiokuwa na vibali ambao hivi karibuni walifukuzwa nchini Tanzania wakiendelea kukwama katika maeneo ya mipakani, kumezuka hali ya wasiwasi juu ya majaliwa hayo. 

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limesema wahamiaji hao kutoka nchi za Rwanda, Uganda na Burundi wapo katika hali mbaya kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo waliyokwama. 

IOM imesema kuwa wengi wa wahamiaji hao ikiwemo watoto na wanawake wanakabiliwa na tishio la kukubwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na maeeo yaliyokwama kukosa huduma muhimu. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM:

(Sauti ya Jumbe Omari Jumbe)