Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugonjwa wa Polio waanza kudhibitiwa eneo la Pembe ya Afrika

Ugonjwa wa Polio waanza kudhibitiwa eneo la Pembe ya Afrika

Kumekuwa na mafanikio ya kukabiliana na ugonjwa wa kupooza uliolipuka katika eneo la pembe ya Afrika miezi sita iliyopita ambao uliathiri watoto kiasi cha 2000 na watu wazima kadhaa.

Maeneo yaliyopigwa na ugonjwa huo ni pamoja na Somalia, Kenya na Ethiopia. Ripoti zinaonyesha kuywa maeneo mengi yaliyokumbwa na tatizo hilo sasa yameanza kupata afuani kutokana na juhudi kubwa zilizochukiliwa na serikali kwa kushirikiana na nchi wahisani.Lakini hata hivyo bado kumesalia hali ya hatari katika baadhi ya maeneo . George Njogopa na ripoti kamili.

(Taarifa ya George)

Kwa mujibu wa takwimu kuhusiana na ugonjwa huo, zinaonyesha kuwepo kwa mafanikio makubw yaliyopatikana nchini Somalia ambayo iliathiriwa vibaya na ugonjwa huu baada ya kuanzishwa kampeni ya utoaji chanjo iliyosambazwa katika maeneo mbalimbali.

Kampeni hiyo iliyoanza kufanywa kunzia mwezi Julai huko Banadir imefanikisha kupunguza kiwango cha ugonjwa huo kwa kiwango kikubwa. Hali hiyo ya mafanikio imejitokeza pia katika nchi za Kenya na EthiopiaKulungana na mwakilishi mkazi shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF Bwana Steven Allen,amesema kuwa pamoja na kupatikana kwa mafanikio hayo lakini hata hivyo bado kumesaliwa na jukumu kubwa mbele.

Amesema mamlaka zinazohusika pamoja na wananchi kwa ujumla hawapaswi kubweteka na mafanikio hayo yaliyoajitokeza bali wanapaswa kukaza mkwiji ili kuhakilisha kwamba kitisho hicho cha kupooza kunaondoshwa kabisa katika eneo hilo.