Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi, maafikiano yacheleweshwa na malumbano

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi, maafikiano yacheleweshwa na malumbano

Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia kikielekea mwisho taarifa zinasema hali ni tete katika mijadala ambapo mabishano yameibuka kati ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea . Malumbano hayo yamesababisha vikao kufanyika hadi usiku wa manane na wakati mwingine baadhi ya wawakilishi kutoka nje kama ishara ya kutokubaliana na mapendekezo au  hoja.

Kutaka kufahamu kulikoni, Joseph Msami wa idhaa ya Kiswahili ya radio ya Umoja wa Mataifa amezungumza na  Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na taaluma ya mkataba huo Dk. Richard Muyungi na hapa anaanza kwa kueleza naman mkataba wa Kyoto ulivyoshindwa kutimiza malengo yake.

 (Sauti Dk Muyungi-mahojiano)