Elimu ndio muarubaini wa kutokomeza ugaidi: Blair

Elimu ndio muarubaini wa kutokomeza ugaidi: Blair

Kamati ya Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa ya kupambana na ugaidi imekutana leo ambapo mwasisi wa Tony Blair Faith Foundation, Tony Blair amehutubia kamati hiyo kwa niaba ya tasisi yake kuhusu namna ya kupambana na watekelezaji wa ugaidi kupitia elimu

Akihutubuia mkutano huo Tony Balir ambaye ni waziri mkuu mstaafu wa Uingereza amesema njia pekee ya kupambana na ugaidi katika dunia ya leo ni kuwekeza katika kutoa elimu hususani kwa vijana. Amesema watekelezaji wa vitendo vya ugaidi wanatumia hofu kama mtaji kwa kuwa hofu inatokana na ujinga na akasisitiza.

(Sauti Tony Blair)

Ndio maana nasema katik akarne ya 21 elimu ni suala la usalama, na sio elimu yoyote isipokuwa ile inayofungua fahamu za vijana kwa kiwango cha juu amabo wana tofauti za kitamaduni na kidini na kuwaonyesha kwamba mustakabali ufanyao kazi ni ule ambamo watu wanaheshimiwa bila akujadli dini zao wala utamaduni

Wakati hayo yakijiri hapa mjini New York, baadhi ya watanzania wamezungumza na idha hii kuhusu namna wanavyoulewa ugaidi.

(Sauti watanzania)