Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtandao maalum wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wazinduliwa

Mtandao maalum wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi wazinduliwa

Mwaka mmoja tangu kufanyika kongamano la 18 la mabadiliko ya tabia nchi, ambalo liliagiza kuundwa kwa chombo maalumu kitachomulika masuala ya teknolijia kuhusiana na mazingira, hatimaye mtandao maalumu umezinduliwa rasmi. Taarifa zaidi na George Njogopa:

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)

Mtandao huo ambao unanguvu za kisheria kulingana na mkataba wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, umebuniwa ili kupunguza shughuli za uchafuzi wa mazingira na badala yake kutoa msukumo katika mambo ambayo yanaelezwa ni rafiki wa mazingira hasa katika nchi zinazoendelea.

Chombo hicho cha kitaaalamu kinajumuisha wataalamu kutoka shirika la maendeleo la viwanda la Umoja wa Mataifa UNIDO na taasisi nyingine 11 zinazojihusisha na masuala ya utafiti.

Akizungumzia kuanzishwa kwa chombo hicho, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP Achim Steiner alipongezwa hatua hiyo ambayo ameiitaka kama “ hatua kubwa ya kuelekea kwenye ushindi iliyoanzichwa na nchi wanachama”

Katika mkutano wa kilele wa mabadiliko ya tabia nchi uliofanyika mwaka 2010 huko Cancun, nchi wanachama zilikubaliana kuundwa kwa chombo maalumu ambacho kitakuwa na kazi ya kutoa msaada wa kitalamu kuhusiana na masuala yanayohusiana tabia nchi kwa mataifa yanayoendelea .