Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi Warsaw watafuta njia baada ya Kyoto

Mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi Warsaw watafuta njia baada ya Kyoto

Wakati kikao cha kumi na tisa cha mkutano wa mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabia nchi kinakaribia ukingoni mjini Warsaw, Poland, bado makubaliano tarajiwa yatakayochukua nafasi ya mkataba wa Kyoto ambao haujaweza kudhibiti uchafuzi wa mazingira duniani hayajafikiwa huku ikielezwa malumbano yametawala mkutano baina ya nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea. Mwenyekiti wa Kamati ya dunia ya Kisayansi na taaluma ya mkataba huo Dk. Richard Muyungi ameiambia Idhaa hii kutoka Warsaw kuwa malumbano ni kwamba nchi zinataka mkataba mpya .

(Sauti Dk Muyungi)

Hoja ya nchi zinazoendelea ambayo inakabiliana na mkwamo ninini?

(Sauti Dk Muyungi)

Mkutano huo unamalizika kesho ijumaa huku m akubaliano mapya yanatakiwa yawe yamefikiwa ifikapo mwaka 2015 wakati wa kikao kitakachofanyika mjini Paris, Ufaransa