Ban ashauriana na viongozi pembeni mwa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

21 Novemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amefanya mkutano na washirika kwenye majadiliano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Warsaw Poland kwenye mkutano kuhusu mabadilio ya hali ya hewa ambao umekuwa ukindelea wiki hii. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi.

Taarifa ya Jason Nyakundi

Ban alifanya mazungumzo na mawaziri kutoka kwa jumuia ya visiwa vidogo, mataifa ya G77 na Uchina , Brazil , Afrika Kusini na India. Ban pia alifanya mazungumzo na mjumbe maalum kuhusu masuala ya mabadiliko ya hali hewa kutoka Marekani Todd Stern , waziri wa mazingira nchini Korea Kusini Seong kyu Yoon miongoni mwa mawaziri wa mzingira kutoka Mexico na Iran. Ban ametoa wito kwa mataifa yaliyostawi kuongoza katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa akikisisitiza kuwa kila nchi ni lazima itekeleze wajibu wake. Ban alisisitiza kuwa ni muhimu kufadhili masuala yanayohusiana na hali ya hewa na kutenga fedha zaidi kwenye miradi isiyochafua mazingira.