Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Afya ya watoto yaangaziwa nchini Tanzania

Afya ya watoto yaangaziwa nchini Tanzania

Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya mkataba wa watoto ambapo haki za mtoto huangaziwa, idhaa hii inamulika afya za watoto katika nchi za Afrika Mashariki hususani Tanzania.

Kutokana na takwimu za vifo vya watoto katika mikoa ya kanda ya ziwa kuwa juu, serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii chini ya ufadhili shirika la misaada la kimarekani la USAID limeanzisha na mradi wa kutibu homa, wenye lengo la kupunguza vifo vya watoto ambapo watoto wamekuwa wakipata huduma maalumu na ya haraka kwa kupata vipimo ili kujua chanzo cha homa kabla ya kupatiwa dawa. Ungana na Noel Thomson katika makala ifuatayo

 (MAKALA YA NOEL)