Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake kutetewa ili wajitokeza kwenye sayansi ya Nyuklia

Wanawake kutetewa ili wajitokeza kwenye sayansi ya Nyuklia

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la nguvu za atomiki la Umoja wa Mataifa anatazamia kuzungumzia nafasi ya mwanamke kwenye masuala ya sayansi, wakati atapohutubia hadhara moja mjini New York mwishoni mwa juma. 

Bi Janice Dunn Lee ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo, atagusia umuhimu wa wanake kushiriki kwenye masuala ya sayansi hasa lakini sayansi ya nuklia. 

Kwa miaka mingi wanawake wamekuwa hawapewi fursa kujitokeza kwenye sayansi ya nukilia jambo ambalo limezidi kuongeza pengo kla kijinsia. 

Hotuba yake hiyo inatazamia kutoa mwanga mpwa kwa wanawake na huenda ikamaliza kusumba iliyodumu kwa miaka mingi ya kuwatenga wanawake kwenye maeneo ya sayansi.