Ukosefu wa Ajira bado changamoto kwa uchumi wa nchi zinazoendelea:Ripoti

20 Novemba 2013

Shirika la Umoja wa Mataifa la biashara na maendelo, UNCTAD limetoa ripoti ya nchi zinazoendelea ya mwaka 2013 yenye kauli mbiu, ustawi na ajira kwa maendeleo jumuishi na endelevu. Ripoti hiyo inayobainisha kwamba watu millioni 130 wataingia sekta ya ajira katika nchi zinazoendelea kufikia mwaka 2020, imeangalia uchumi wa  nchi zinazoendelea na uhusiano wake na ajira ambapo impendekeza sera ambazo zitawezesha kuongeza nafasi za kubuni ajira. katika mahojiano maalum na Patrick Maigua wa Radio ya Umoja wa Matifa Mkurugenzi Mkuu wa UNCTAD Mukhisa Kituyi amesema ajira bado ni changamoto inayokumba mataifa yanayostawi

(SAUTI YA MUKHISA)

Katika hatua nyingine Kituyi amesema kuwa jambo la kusikitisha ni kwamba mataifa yanayokabliwa na ukosefu wa ajira yanaongoza katika viwango vya watoto wanaozaliwa hali ambayo inaendelea kugharimu sekta ya ajira sasa na kwa siku za usoni

 (SAUTI YA MUKHISA)

Ripoti hii hutolewa kila mwaka na inalenga mataifa yanayoendelea.