Ban amteua Krähenbühl wa Geneva kuwa kamishina mkuu wa UNRWA

20 Novemba 2013

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemteua Pierre Krähenbühl wa Switzerland kuwa kamishina mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na misaada ya kiutu kwa wakimbizi wa kipalestina UNRWA.

Uteuzi huo unafautia ushauri wa tume ya ushauri ya UNRWA ambapo mteule huyo anachuku anafasi ya Filippo Grandi. Bwana Krähenbühl ana uzoefu mkuu katika masuala ya misaada ya kibinadamu, maendeleo, afya na haki za binadamu pamoja na masuala ya uongozi hususani nai katik maeneo hatarishi.

Ana shahada ya siasa ya sayansi na mahusiano ya kimataifa aliyoipata mwak 1991 mjini Geneva . Amezaliwa mwaka 1966 mjini Geneva na ana mke na watoto watatu.